Netanyahu asikitishwa na mauaji ya wanajeshi wake Gaza
25 Juni 2025Matangazo
Akiandika kwenye mtandao wake wa X, Netanyahu amesema ni masikitiko makubwa kwa watu wa Israel baada ya kuuawa wanajeshi hao aliowaita mashujaa walioangamia katika vita vya kumdhibiti adui Hamas na juhudi za kuachiwa mateka wanaoshikiliwa na kundi hilo kusini mwa Gaza.
Afisa mmoja wa jeshi amesema wanajeshi hao waliuwawa baada ya gari walimokuwa wakisafiria kuripuliwa kwa bomu.
Wanajeshi saba wa Israel wauwawa Gaza
Taarifa hiyo imetolewa siku moja baada ya duru za hospitali Gaza kusema wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi Wapalestina waliokuwa wakisubiri kupokea misaada kusini mwa Gaza hapo jana, na kusababisha mauaji ya Wapalestina 44.