Narendra Modi ahutubia taifa kwa mara ya kwanza
12 Mei 2025Waziri mkuu wa India Narendra Modi amelihutubia taifa jioni hii kwa mara ya kwanza tangu kufikiwa kwa makubaliano na Pakistan,ya kusitisha vita katika jimbo la Kashmir.
Soma pia: India na Pakistan zafungua tena viwanja vya ndege baada ya vita kusitaModi amesema jeshi la India lilipata idhini kamili ya kuyaangamiza makundi ya kigaidi upande wa Pakistan. Hotuba ya kiongozi huyo ambayo ni ya kwanza mbele ya hadhara tangu makubaliano ya Jumamosi ya usitishaji vita yaliyosimamiwa na Marekani , imekuja chini ya kiwingu cha utulivu kiasi kati ya pande hizo mbili.Soma pia: Wanajeshi wa Pakistan na India washambuliana huko Kashmir
Mamlaka za mataifa yote mawili zimefahamisha leo Jumatatu,kwamba hakuna mashambulizi yaliyoripotiwa usiku wa kuamkia leo kwenye maeneo ya Jammu na Kashmir.