François Bayrou awasihi wabunge kutumia busara kura ya imani
8 Septemba 2025Matangazo
Akizungumza wakati wa kikao cha bunge, waziri mkuu huyo amewataka wabunge wauunge mkono mpango wake wa kupunguza deni kubwa la taifa analosema "linaididimiza Ufaransa.”
Bayrou ameonya kuwa nakisi ya bajeti na madeni yanayoongezeka vinatishia mustakabali wa uchumi wa taifa hilo, ambao ni wapili kwa ukubwa katika Umoja wa Ulaya, huku wachambuzi wakitabiri kuwa atalazimika kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Rais Emmanuel Macron iwapo kura hiyo itampinga.
Hii itakuwa mara ya tatu kwa Ufaransa kubadilisha Waziri Mkuu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.