Murkomen: Maandamano yaliyofanyika Kenya yalikuwa ugaidi
26 Juni 2025Matangazo
Katika hotuba yake aliyoitoa kwa njia ya televisheni, Kipchumba Murkomen amewatuhumu waandamanaji kwa kujaribu kufanya mapinduzi dhidi ya serikali.
Soma zaidi: 16 wauawa kwenye maandamano ya GenZ nchini Kenya
Amewalaani wahalifu walioyatumia maandamano hayo kufanya vurugu, uporaji, unyanyasaji na uharibifu. Watu 16 wameuawa katika maandamano hayo kulingana na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International.
Maandamano hayo yaliyohusisha maelfu ya raia yalilenga kuadhimisha mwaka mmoja tangu yalipofanyika maandamano ya kuupinga muswada wa ongezeko la kodi ambapo takriban watu 60 waliuawa.