Faeser apongeza mafanikio ya Ujerumani kudhibiti uhamiaji
1 Aprili 2025Matangazo
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser amesema serikali ya mseto imefanya kazi nzuri kuhusu uhamiaji huku kukiwa na shinikizo la kisiasa kwa vyama vikubwa vya siasa kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaoingia.
Akizungumza katika mkutano kuhusu uhamiaji haramu uliowakusanya wajumbe kutoka nchi 40 jijini London, Uingereza, waziri huyo alihimiza kupunguza malumbano katika mdahalo kuhusu sera ya uhamiaji na uombaji hifadhi ya siku za usoni, akiongeza kwamba changamoto hazitatatuliwa kwa tabia ya kupotosha na hila.
Faeser amesema serikali inayoondoka ya Ujerumani imefanikiwa kuleta uwiano katika kudhibiti uhamiaji usio wa kawaida lakini pia kuimarisha taswira ya kuvutia ya Ujerumani kama mahala pa wafanyakazi wenye ujuzi kuhamia.