Chanjo dhidi ya malaria imeanza kutolewa nchini Uganda huku mamlaka za afya zikitanguliza zoezi hilo katika wilaya ya Apac, kaskazini mwa nchi, inayosemekana kuwa na kiwango cha juu cha mbu walio na vijidudu. Chanjo hii inatolewa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka miwili kwa awamu nne.