Wazawa hutoa nyaraka zao kusajili biashara za Wachina K'Koo
19 Machi 2025Soko la Kariakoo, ni eneo linalojulikana kama kitovu cha biashara jijini Dar es Salaam, lakini hali ya wasiwasi inaongezeka kati ya wafanyabiashara wazawa. Malalamiko yanazidi kusikika kuhusu namna raia wa kigeni, hususan Wachina, wanavyohodhi biashara, na kuwapiku wafanyabiashara wa Kitanzania.
Manka Mushi, mfanyabiashara wa Kariakoo, anasimulia akisema kwamba, "ukienda kwao kununua unanunua kwa bei ile wanayouza wao, nikiileta sokoni lazima niongeze kidogo, nikiongeza na wao wanauza kwa bei ile ile kwa sababu wanakuwa na meza zao hapa hapa.” Serikali ya Tanzania yaunda tume na wafanyabiashara
Februari 4 mSerikali ya Tanzania yaunda tume na wafanyabiasharawaka 2024, Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania, Seleman Jaffo, aliunda kamati ya watu 15 kuchunguza mazingira ya wafanyabiashara wa kigeni wanaofanya biashara za wazawa katika soko la kimataifa la biashara la Kariakoo.
Ripoti ya kamati hiyo iliyoongozwa na Profesa Eda Lwoga, ilibaini kuwa, biashara nyingi zinazomilikiwa na raia wa kigeni, hasa wa China, zimesajiliwa kwa kutumia nyaraka za wazawa, anasema Waziri Jaffo. Waziri huyo ameongeza kuwa, "na hasa mlivyotembelea wafanyabiashara, na mkabaini kwamba biashara nyingine japo zinaonekana ni za wageni lakini nyaraka zinaonyesha zinamilikiwa na watanzania."Wafanyabiashara katika soko la kariakoo, Tanzania walalamikia kunyanyaswa na mamlaka za jiji la Dar es Salaam.
Jaffo alichukua hatua hiyo baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupokea malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara hao juu ya kuwepo kwa wafanyabiashara wa kigeni wanaowazidi nguvu wafanyabiashara wazawa.
Mfanyabiashara katika soko la Kariakoo, Athuman Mohamed, anasema wamepinduliwa na Wachina walioihodhi Kariakoo: "Mzawa huwezi kuuza kwasababu mtu wa kawaida anayekaa Tabata, nanunua kwa mchina, omba Mungu upajue kwa Mchina,ukiwa na elfu kumi yako unalipa unachukua, mchina ubaya wake anauza bei ya jumla hiyo hiyo na reja reja hiyo."
China ni mwekezaji namba moja hapaTanzania ambapo mwaka 2019, mtiririko wa Uwekezaji wa Moja kwa Moja wa Kigeni (FDI) kutoka China ulifikia dola za Kimarekani milioni 115. Aprili 2021, kampuni 800 za China zilikuwa tayari ziwekeza katika taifa hili la Afrika ya Mashariki.
Hata hivyo, kufuatia ripoti ya kamati hiyo iliyoundwa na serikali, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara na Huduma Tanzania, (Uwahuta) Martin Mbwana, ameishauri serikali kuwa badala ya kuwawekea vizuizi raia wa kigeni, itoe elimu zaidi kwa wazawa:
"Tulichokuwa tunashauri tufanye juu chini, kwa sababu elimu ni vita, tupambane tuwape elimu wafanyabiashara wenzetu namna ya kuwa shareholders, kwa ushirika”
Soma pia: Jengo laporomoka Kariakoo, Dar es Salaam
Hoja ya ikiwa suluhisho ni kuwapiga marufuku wafanyabiashara wa kigeni au kuwawezesha wazawa ili waweze kushindana katika mazingira haya mapya inananing'inia hewani, wakati ambapo soko la Kariakoo likiendelea kuwa kiini cha biashara na mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.