MigogoroAfrika
Wawakilishi wa serikali ya Kongo, M23 wakutana Qatar
6 Aprili 2025Matangazo
Chanzo chenye ufahamu na suala hilo kimearifu Jumamosi kuwa mazungumzo hayo yaliyolenga kupata mwafaka wa kusitisha mapigano mashariki mwa Kongo yalifanyika kwa faragha Alhamisi.
Soma zaidi: Kongo na waasi wa M23 kuanza mazungumzo ya ana kwa ana
Hii ni mara ya kwanza kwa pande mbili za mzozo huo kukutana ana kwa ana baada ya muda mrefu. Mazungumzo zaidi ya usuluhishi yanatarajiwa kufanyika tena Doha nchini Qatar ili kuimarisha juhudi za kutafuta suluhisho la mgogoro kati ya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi wa M23.
Waasi hao wanadhibiti maeneo makubwa ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini na wameiteka miji mikuu ya mikoa hiyo, Bukavu na Goma tangu mwezi Januari mwaka huu.