MigogoroMashariki ya Kati
Hamas waelekea Misri kwa mazungumzo ya kusitisha vita Gaza
12 Aprili 2025Matangazo
Afisa wa Hamas mwenye ufahamu na mazungumzo hayo aliyeomba asitajwe jina amesema kundi hilo lina matumaini kuwa majadiliano hayo yatapiga hatua ili kupata makubaliano ya kumaliza kabisa vita. Kulingana na afisa huyo ujumbe wa Hamas unaongozwa na msuluhishi mkuu wa kundi hilo Khalil al-Hayya.
Soma zaidi: Wapatanishi wapambana kunusuru makubaliano ya Gaza
Pamoja na hatua hiyo, chanzo cha taarifa hii kimethibitisha kuwa wanamgambo wa Hamas bado hawajapokea mapendekezo yoyote mapya ya kusitisha vita, licha ya vyombo vya habari vya Israel kudai kuwa nchi hiyo imebadilishana na Misri nyaraka zinazoainisha makubaliano muhimu ya kusitisha vita na kuwaachilia huru mateka.