MigogoroMashariki ya Kati
Vita vyaendelea Gaza, Wapalestina waandamana kuipinga Hamas
3 Aprili 2025Matangazo
Umoja wa Mataifa umesema kuwa katika muda wa siku mbili zilizopita, zaidi ya watu 100,000 wa kusini mwa Gaza wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulizi ya Israel.
Soma pia: Wapalestina wachoshwa na kuhamishwa kila mara kwenye makazi yao
Hayo yanajiri wakati maandamano mengine makubwa yameshuhudiwa huko Gaza yakiupinga utawala wa Hamas na kulaani vita hivyo vilivyodumu kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa. Taarifa za hivi punde zinaeleza kuwa Hamas wametupilia mbali pendekezo la hivi punde la Israel kuhusu usitishaji mapigano.