MigogoroUlaya
Watu wawili wauawa Ukraine kufuatia mashambulizi ya Urusi
22 Machi 2025Matangazo
Mashambulizi hayo yameripotiwa katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Ukraine la Sumy na pia katika miji mingine ya Ukraine ikiwa ni pamoja na mji mkuu Kiev.
Meya wa mji wa Kiev Vitali Klitschko ametoa wito kwa raia kutafuta maeneo ya kujikinga na mashambulizi hayo.
Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa, Ukraine imekua ikipambana na uvamizi wa Urusi, huku Marekani chini ya utawala wa rais Donald Trump ikiwa imeanzisha mchakato wa mazungumzo ya kuutafutia suluhu mzozo huo.