MigogoroMashariki ya Kati
Watu wawili wauawa katika mashambulizi ya Israel Rafah
19 Februari 2025Matangazo
Jeshi la Israel limesema shambulizi hilo lilikuwa la kujihami dhidi ya mtu aliyekataa kutii amri ya kutovisogelea vikosi vyake na kwamba wamefanya operesheni kadhaa katika maeneo mengine huko Gaza dhidi ya washukiwa ambao walionekana kuwa tishio.
Soma pia:Umoja wa Ulaya wapeleka ujumbe wa kiraia kwenye kivuko cha Rafah
Mashambulizi hayo yameripotiwa licha ya kuwepo makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na kundi la Hamas ambalo limetangaza hapo jana kuwa litawaachia mateka sita wa Israel siku ya Jumamosi na miili ya mateka wengine wanne Alhamisi wiki hii, kama sehemu ya kutekeleza makubaliano hayo.