Watu watatu wauawa Urusi kwa shambulio la Ukraine
9 Julai 2025Shambulizi la droni la Ukraine limewauwa watu watatu, akiwemo askari katika mji wa Kursk wa Urusi, karibu na mpaka na Ukraine, hayo yamesemwa na kaimu gavana wa eneo hilo Alexander Khinshtein.
Kiongozi huyo amevishutumu vikosi vya Ukraine kwa kufanya mashambulizi hayo aliyoyaita kuwa yasiyo ya kibinadamu na kwamba vikosi hivyo vilishambulia kwa makusudi maeneoya raia.
Katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv, Urusi nayo imefanya mashambulizi ya droni ambapo mamlaka katika mji huo zimesema shambulio moja limemjeruhi mwanamke mmoja.
Vita hivyo vya zaidi ya miaka mitatu mpaka sasa havionyeshi dalili zozote za kumalizika licha ya jitihada mbalimbali ikiwemo shinikizo kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump ambaye hivi karibuni amesema nchi yake itaitumia silaha zaidi Ukraine ili iweze kujilinda na mashambulizi ya Urusi.