MigogoroUlaya
Mashambulizi ya Urusi yawaua raia watatu wa Ukraine
1 Februari 2025Matangazo
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ukraine imesema watu wawili wameuawa na wengine saba wamejeruhiwa katika mji wa Poltava baada ya jengo la makazi kushambuliwa kwa kombora. Mtu mmoja ameuawa katika mji wa kaskazini mashariki wa Kharkiv.
Soma zaidi: Shambulio la droni la Urusi laua watu tisa mashariki mwa Ukraine
Haya yanajiri wakati rais wa Marekani Donald Trump ametangaza jana jioni kuwa utawala wake tayari umefanya mazungumzo "makubwa" na Urusi kuhusu vita vya Ukraine, na kwamba yeye na Rais Vladimir Putin wa Urusi wanaweza kuchukua hatua "muhimu" hivi karibuni kuumaliza mzozo huo.
Tangu aliporejea madarakani, Trump amemkosoa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelenskiy, akisema kuwa alipaswa kufikia makubaliano na Putin ili kuepusha vita.