Israel yashambulia Kanisa Katoliki pekee huko Gaza
18 Julai 2025Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameelezea masikitiko yake baada ya shambulizi la Israel dhidi ya kanisa pekee la Kikatoliki kuwaua watu watatu na kuwajeruhi watu wengine huko Gaza siku ya Alhamisi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki wa Jimbo kuu la Jerusalem alisema watu wengine 10 pia walijeruhiwa katika shambulio dhidi ya Kanisa la Familia Takatifu mjini Gaza, akiwemo padri wa parokia hiyo.Shambulizi la Israel katika kanisa Katoliki Gaza laua watu wawili
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo wa XIV(14) ameelezea kuhuzunishwa na mauaji hayo na kutoa wito wa usitishaji mapigano mara moja huku pia akielezea matumaini yake makubwa ya mazungumzo na maridhiano ya upatikanaji wa amani ya kudumu katika kanda hiyo.
Ikulu ya White House imesema Rais Donald Trump "hakuwa" na "majibu chanya" kuhusu shambulizi la Israeli dhidi ya kanisa la Kikatoliki pekee la Gaza.