MigogoroUkraine
Watu watatu wauawa katika shambulio la droni mjini Kyiv
23 Machi 2025Matangazo
Meya wa jiji la Kyiv Vitali Klitschko, na msimamizi wa kijeshi Teymur Tkachenko, wamesema mashambulizi ya droni yalifanyika usiku kucha, na yalisababisha moto kwenye magorofa kadhaa. Ving'ora vilisikika angani katika mji mkuu wa Ukraine kwa zaidi ya saa tano za mashambulizi.
Tkachenko amesema, mtoto wa miaka mitano ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha, na mtoto mwingine wa miezi 11 alijeruhiwa.
Mashambulio hayo yametokea huku wapatanishi wa Marekani wakitarajiwa kukutana Jumatatu (24.03.2025) na wajumbe wa Ukraine na Urusi nchini Saudi Arabia, kujadili uwezekano wa kusitisha mapigano. Urusi iliahidi kusitisha mashambulizi dhidi ya miundombinu ya nishati ya Ukraine, kufuatia mazungumzo wiki hii kati ya Vladimir Putin na Donald Trump.