MigogoroMashariki ya Kati
Wapalestina 35 wauawa katika mashambulizi Ukanda wa Gaza
26 Juni 2025Matangazo
Mamlaka za afya za Gaza zimesema miongoni mwa waliouwawa ni watu tisa wameuawa kwa mashambulizi ya anga katika shule inayozihifadhi familia zisizo na makazi kwenye eneo la Sheikh Radwan.
Soma zaidi: Gaza: Watu zaidi wauawa kwenye mashambulizi ya Israel
Shambulio jingine limewaua watu wanane karibu na mahema kwenye kambi moja mjini Khan Younis. Watu wengine kadhaa wameuwawa wakati wakisubiri msaada wa chakula kutoka katika malori ya Umoja wa Mataifa.
Mashambulizi haya yametokea wakati wasuluhishi wakifanya juhudi za kuwasiliana na wawakilishi wa Israel na kundi la Hamas ili kufufua majadiliano ya kusitisha mapigano kwa lengo la kuvimaliza vita.