Watu wasiopungua 20 wauawa katika mashambulizi Gaza
14 Agosti 2025Wapalestina wasiopungua 20 wameuawakatika wimbi la mashambulizi ya Israel Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa vyanzo vya ndani. Miili ya watu hao ilipelekwa katika hospitali mbili za Nasser na Awda.
Mashuhuda na wafanyakazi wamelieleza shirika la habari la AFP kwamba baadhi ya watu waliokufa walikuwa wamepigwa risasi wakati wakielekea vituo vya kugawa misaada au wakati wakisubiri misafara inayoingia Gaza. Wengine, wakiwemo watoto watano, walifariki wakati shambulizi la anga lilipogonga hema lao katika mji wa Gaza.Israel yaidhinisha mashambulizi mapya Gaza
Shirika la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kaskazini mwa Gaza yamesababisha kifo cha mtu mmoja, kwa mujibu wa madaktari, huku watu watano wakiuawa wakati wakisubiri msaada kusini mwa Wadi Gaza katikati mwa eneo hilo, .