Watu tisa wafariki katika shambulio huko Iraq:
25 Januari 2004Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq wameuawa watu tisa katika orodha ya mashambulio. Liliporipuliwa bomu ndani ya gari mjini Samarra hapo jana waliuawa Wairaq wanne na kujeruhiwa watu wengi wengine. Wanajeshi watatu wa Kimarekani waliuawa katika shambulio la bomu mjini Kahldijah. Wanajeshi wawili wengine wa Kimarekani waliuawa katika shambulio karibu ya mji wa Falluja. Wanajeshi wa Kimarekani wanashutumu kuwa orodha hiyo ya mashambulio imefanywa ama na wafuasi wa Rais aliyepinduliwa Saddam Hussein au yameandaliwa kutokea nje ya nchi.