Watu takriban 18 wauwawa Ukraine
24 Juni 2025Matangazo
Urusi imefanya mashambulio ya droni na makombora dhidi ya Ukraine, na kusababisha vifo vya kiasi watu 18 na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa.
Maafisa wa Ukraine wamesema vikosi vya Urusi vimekuwa vikifanya mashambulio mfululizo dhidi ya maeneo ya makaazi ya raia nchini Ukrainetangu vita vilipoanza miaka zaidi ya mitatu iliyopita. Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya raia 12,000 wa Ukraine wameuliwa kwenye vita hivyo.
Mashambulio hayo yamefanyika wakati rais Volodymyr Zelensky anatafuta njia ya kuhakikishiwa kupata msaada zaidi wa kijeshi kutoka mataifa ya Magharibi kukabiliana na uvamizi huo wa Urusi.
Zelensky anajiandaa kukutana leo na viongozi wa nchi za Magharibi wanaoshiriki mkutano wa Jumuiya ya kijeshi ya NATO nchini Uholanzi.