MigogoroUkraine
Watu saba wauawa kwenye mashambulizi ya Urusi nchini Ukraine
3 Agosti 2025Matangazo
Kwa mujibu wa mamlaka za serikali za mitaa, watu watano waliuawa na wengine 11 kujeruhiwa katika miji kadhaa ya Donetsk na katika mkoa wa Kherson, watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 10 kujeruhiwa.
Maafisa wamesema mji wa Kherson ambao bado uko chini ya udhibiti wa Ukraine, ulishambuliwa mapema leo asubuhi wakati jana Jumamosi kuliripotiwa mashambulizi yaliyosababisha uharibifu wa daraja la kuvukisha magari, bomba la kusafirisha gesi na magari kadhaa.
Urusi imevamia sehemu kubwa ya mikoa yote miwili ya Donestk na Kherson na inaendeleza juhudi za kuikamata kabisa.
Kampeni ya kijeshi ya Urusi imekuwa ikilenga sana maeneo ya mashariki na kusini mwa Ukraine.