MigogoroMashariki ya Kati
Watu kadhaa wauawa Gaza kufuatia mashambulizi ya Israel
24 Agosti 2025Matangazo
Wakati huo huo, kumeripotiwa pia mashambulizi katika maeneo ya mashariki na kaskazini mwa mji huo wa Gaza katika vitongoji vya Zeitoun, Shejaia na Sabra huku majengo kadhaa yakiripuliwa katika mji wa kaskazini wa Jabalia.
Shirika la habari la Palestina WAFA limeripoti kuwa mpigapicha wa kituo cha Televisheni cha Palestina Khaled al-Madhoun ameuawa hapo jana kwa kupigwa risasi karibu na kivuko cha Zikim. Chama cha Waandishi wa Habari wa Palestina kimeeleza kusikitishwa na tukio hilo na kikisema kwamba hiyo ni "kampeni inayoendelea ya Israel dhidi ya waandishi wa habari na yenye lengo la kunyamazisha simulizi za Wapalestina."