JamiiCanada
Watu kadhaa wauawa baada ya gari kuvurumishwa kwenye umma
27 Aprili 2025Matangazo
Haya yamesemwa jana jioni na polisi nchini humo huku watu wengine kadhaa pia wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Katika chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa X, polisi imesema kuwa dereva wa gari hilo mwenye umri wa miaka 30 kutoka Vancouver, anayejulikana na polisi, alikamatwa katika eneo hilo la tukio.
Mashuhuda wameeleza kuwa dereva huyo alijaribu kutoroka lakini akakamatwa na wapita njia.
Soma pia: Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney aitisha uchaguzi
Msemaji wa polisi amethibitisha kuwa hakuna hatari zaidi kwa umma.
Meya wa mji wa Vancouver Ken Sim amesema ameshtushwa na kusikitishwa na tukio hilo la kutisha.
Waziri mkuu wa nchi hiyo Mark Carney, pia ameelezea kusikitishwa kwake na tukio hilo kwenye ujumbe aliouchapisha katika mtandao wa X.