Watu kadha wauawa katika shambulio la mabomu Iraq
22 Novemba 2003Matangazo
BAGHDAD: Nchini Iraq, watu si chini ya 15 wameuawa na wengine kadha kujeruhiwa hii leo katika mashambulio mawili ya mabomu. Maafisa wa serikali waliarifu kuwa mashambulio hayo mawili yalifanyika karibu wakati mmoja katika mji wa Baakuba na katika mji mdogo wa Khan Bani Sad, Kaskazini-Mashariki mwa Baghdad. Katika mashambulio hayo vilipigwa hasa hasa vituo vya polisi wa Kiiraq. Inasemekana mji wa Baakuba ndiyo ngome kuu ya wapiganaji wa upinzani dhidi ya majeshi ya Kimarekani. Nayo ndege ya mizigo ya kiraiya ilipigwa na kombora ilipokuwa njiani kutuwa katika uwanja wa ndege wa Baghdad. Watu walioshuhudia wameripoti kuwa bawa mmoja la ndege hiyo ilishika moto baada ya kushambuliwa. Lakini rubani wake aliweza kuitua salama ndege yake hiyo.